Na Oyuke Phostine Filemon
Kituo cha kuchakata na kuzalisha umeme kwa njia ya gesi cha Kinyezi I kimekamilika kwa asilimia 88 na kinatarajiwa kuzalisha umeme kuanzia Septemba mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Meneja Mradi wa Kinyerezi I kutoka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Mhandisi Simon Jilima akiwatembeza katika kituo hicho wanajopo la ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango walipotembelea mradi huo.
“Kazi zinazoendelea kwa sasa ni ufungaji wa mifumo katika mitambo; na njia za kusafirisha umeme msongo wa kV 220 kutoka Kinyerezi hadi Kimara na kV 132 Kinyerezi hadi eneo la viwanda la Gongolamboto, alisema Mhandisi Jilima.
Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Raisi Tume ya Mipango, Bibi. Florence Mwanri, alisema iwapo mradi huu utakamilika na kuanza kuingiza umeme wake katika gridi ya taifa ni dhahiri kuwa gharama za uendeshaji wa viwanda na uzalishaji wa bidhaa zitashuka, na pia kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.
“Katika miaka mitano ijayo mpango wetu wa maendeleo umejikita zaidi katika uchumi wa viwanda hivyo ni vema ujenzi huu ukamilika kwa wakati ili kutoleta changamoto katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa mwaka 2016/17-2020/21” alisisitiza Bibi. Mwanri.
Ili kuongeza uzalishaji wa nishati hiyo tayari Tanesco wameshanunua mitambo mingine mine ambayo itazalisha umeme kiasi cha kV 180.
Sehemu za mashine za kuzalishia umeme wa gesi ambazo ziko tayari katika kituo cha Kinyerezi. |
Mwonekano wa kituo cha kuzalisha umeme wa gesi Kinyerezi kwa juu. |
No comments:
Post a Comment