Kamati ya Kudumu ya Bunge, Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC) ilifanya ukaguzi wa ukarabati wa Reli ya Kati katika Wilaya ya Kilosa kwa kutumia Kiberenge 07/01/2015. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Zitto Zuberi Kabwe (MB) amesema "Zinahitajika tshs 500 bilioni kila mwaka kwa miaka 3 mfululizo kuweza kukarabati miundombuni ya Reli Tanzania ( Reli ya ratili 80 ). Ili kujenga Reli mpya kabisa ya ' standard gauge' zinahitajika $6.5bn .Kwa Nchi kama yetu, bila mtandao wa Reli madhubuti, Uchumi utakua kwa mwendo huu huu wa jongoo badala ya ukuaji wa kasi"
No comments:
Post a Comment