Friday, January 31, 2014

UHABA WA MAJI MOROGORO, MTO MLALI HATARINI KUTOWEKA.

Wajumbe wkiwa waangalia ukaukaji wa Mto Mlali eneo la barabara ya Mzumbe.
Wakazi wa Manispaa ya morogoro wamekuwa wakilalamika kuwa maji hayatoshi huku lawama zikielekezwa moja kwa moja kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (MORUWASA) kuwa haiwapi maji ya kutosha badala yake kupata maji kwa mgao. Lakini ukweli ni kwamba mgao unakuwa mkali zaidi kutokana na upungufu wa maji unaokuwa katika Bwawa la Mindu linalopokea maji kutoka katika mito 5 ambayo ni Mto Mlali, Mzinga, Lukurunge, Migera na Ngerengere.
 Kutokana na uchafuzi wa Mazingira, Uchepushaji wa maji katika mito hii, shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji ni sababu mojawapo zinazofanya maji yawe si ya kutosha.
Ofisi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu ni ofisi yenye jukumu la kusimamia rasilimali maji katika Mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma. Kila mtu kabla hajatumia maji lazima aombe kibali kutoka Ofisi hii.
Bodi ya Ofisi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu iliamua kufanya ziara kuangalia changamoto zinazokabili vyanzo vya maji na ziara hiyo ilikuwa mahsusi kwa mto Mlali.

Wajumbe wa Bodi ya Ofisi ya Maji Bonde la Wami/Ruvu wakiwa katika Kiwandana Cha Nguo Cha 21st Century textiles Ltd wakisikiliza Maelezo kutoka kwa Meneja Uzalishaji wa Kiwanda hicho ndg. Munishi.

Bomba la majitaka kutoka Mabwawa ya majitaka ya Viwandani likiwa linamwaga maji mto Ngerengere.

Mto Mlali ukiwa umekauka kutokana na uchepushaji maji usiorasimi unaofanywa na wananchi pamoja na uchafuzi wa Mazingira.

Wajumbe wakiwa eneo la Mto Ngerengere ambako ni eneo maji taka yanayotoka katika mabwawa ya viwandani yanamwagwa.


Mwenyekiti wa Bodi Bw. Mutayoba Washington akiwa anaongea na Mwenyekiti wa umoja wa watumiaji maji (Water Users Association) Mlali 

Kalvat la mto Mlali likiwa limeziba na kukiwa hakuna maji yoyote yanayo tiririka kuelekea bwawa la Mindu ambalo linategemewa na wakazi wa Manispaa ya Morogoro kwa zaidi ya asilimia 70.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya maji Bonde la Wami/Ruvu akiwa anapata maelezo kutoka kwa Ofisa wa Maji Bonde la Wami/Ruvu Bibi. Praxeda Kalugendo. Kushoto ni mjumbe wa Bodi Mhandisi Rutakyamilwa.

Shughuli za kibinadamu zikiendelea katika Mto Mlali.

Uchepushaji wa Mto Mlali maji yakiwa yamezuiliwa kuelekea Bwawa la Mindu na kuelekezwa kwenye mashamba ya umwagiliaji.

Wajumbe wakijadiliana jambo

Wajumbe wa Bodi ya Ofisi ya Maji bonde la Wami/Ruvu  wakiwa wanaendelea na ziara yao katika mto Mlali Wilayani Mvomero

Mlima Uluguru unavyoonekana kwa mbali

Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Maji bonde la Wami/Ruvu akiwa anawaelimisha wakazi wa Mlali kutoendelea kuchafua vyanzo vya maji.

Mto mlali ukiwa umekauka

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...