Monday, December 31, 2012

HERI YA MWAKA MPYA 2013.

MWENYEZI MUNGU MWENYE KUWEZA KILA JAMBO,AMEWEZA KUKUONGOZA VIZURI MPAKA SASA UNAPUMUA. Una kila sababu ya kumshukuru kwa kila jambo.Niwengi waliuanza huu mwaka wa 2012 lakini katikati safari zao zikakatishwa na uhai wao kuweza kuchukuliwa.

Jiulize kwa mwaka 2012 umefanya nini la kumtukuza mwenyezi mungu,umefanya nini la kuisaidia jamii.Ukishafanya tathimini hiyo jipe jibu na kuweza kujikosoa.

Wengi tunalalamika kuwa hatuna kitu,lakini kusaidia ni moyo sio utajiri.Mtu mwingine unaweza kumsaidia mawazo na akaweza kukwamuka kimaisha.

Nawaomba tupendane wote madamu tunaishi,sote ni ndugu.


DAR ES SALAAM YATOLEWA KAFARA KWENYE DIJITALI.

Waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Prof.Makame Mbarawa.


MKOA wa Dar es Salaam saa 6 kamili usiku wa leo unakuwa wa kwanza kuzimiwa mitambo ya analojia ya utangazaji wa televisheni kwa ajili ya kupokea mfumo mpya wa digitali.

Ikumbukwe kuwa hatua hiyo ya kuhama kutoka analojia kwenda digitali ni utekelezaji wa makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa katika hotuba yake ya jana kuashiria uzimaji wa mitambo ya analojia, alisema uzimaji kwa zamu unalenga kuepusha usumbufu kwa wananchi wa Tanzania.

Mbarawa alisema kuwa mchakato huo wa uzimaji wa mitambo utafanyika kama ifuatavyo: Januari 31, 2013 Dodoma na Tanga. Mkoani Mwanza Februari 28, 2013 na Kilimanjaro (Moshi) na Arusha Machi 31, 2013.

Mkoa wa saba kuingia kwenye mfumo wa digitali utakuwa Mbeya ambao mitambo itazimwa Aprili 30, 2013. Utaratibu wa kuzima mitambo ya analojia utakuwa kwa maeneo yenye matangazo ya digitali na kwa yasiyo na miundombinu ya digitali hayatazimwa.

Taarifa ya Waziri inaonesha kwamba miundombinu ya mitambo ya digitali imeenea katika mikoa minane pekee. Mabadiliko hayo yanahusu matangazo kwa njia ya utangazaji wa satelaiti, waya (cable) na redio.

Aidha imeelezwa kwamba watoa huduma za miundombinu ya digitali wamejipanga kusimika mitambo hiyo katika mikoa mingine minane ndani ya miezi minane ijayo.
Lakini kwa upande wa pili wa shilingi,baadhi ya wananchi wanalalamikia ving'amuzi vingine vunakatakata sana mawasiliano,lakini naona ni changamoto.


Friday, December 28, 2012

UZURI NA MAAJABU YA BUKOBA

Bukoba ni sehemu mojawapo ambayo kila mmoja anapenda akaishi kutokana na uzuri wake.Kihistoria,Bukoba ni sehemu miongoni mwa sehemu barani Afrika ambayo ilitawaliwa na Utawala wa Machifu (WAKAMA).Miongoni mwa machifu hao ni Mukama Lukamba ambaye alikuwa "Chief" wa Kyamutwara makao makuu yake ni Kabale,kata ya Karabagaine.

Nyumbani kwa Mukama Lukamba.



Kwa Wakama  hawa kulikuwa na mahakama (GOMBOLOLA) ambazo zilikuwa zinatumika kuhukumu waarifu wote waliokuwa wanaletwa mahakamani hapo.

Chief Lwaijumba local court
Mahakama ya Mukama Lwaijumba ambapo waarifu walikuwa wanahukumiwa.
Hata hivyo baada ya hukumu hiyo wote waliokuwa wanaadhibiwa kwa kunyongwa sehemu inayoitwa Mlima wa Lyankumbi ulioko Itahwa walipokuwa wanaachiwa na kuporomokwa hadi bondeni.
Mlima Lyankumbi ampako waarifu walikuwa wanaanyongwa.

Pamoja ni hayo,Kabale kuna pango ambalo lilitumika kwa wananchi kujificha wakati wa vita ya Kagera.Pango hilo lina urefu usiopungua kilometa 3.Pango hili la maajabu lipo katika mlima Rwamrumba.
Picha zifuatazo ni picha zinazoonesha pango la maajabu.




Mnamo miaka ya 1977 hadi 1979 kulikuwa na vita ya Kagera,vita hivi vilifanyika hasa maeneo ya Mutukura,Bunazi na Kyaka.Miongozi mwa uharibifu uliofanyika wakati wa vita ni Kuunguzwa kwa kiwanda cha sukari cha Kagera,Kuunguzwa kwa makanisa pamoja na mashule.
Picha zifuatazo ni baadhi tu ya picha zinazoonesha uharibifu uliofanywa na Nduli Iddi Amini -DADA kwa kuunguza kanisa la Kyaka.


Kanisa la Kyaka lililoungua.







Friday, December 21, 2012

CHADEMA WAZIDI KUCHANJA MBUGA,GODBLESS LEMA ASHINDA RUFAA.



  Mbunge wa Arusha mjini Godbless lema ameshinda rufaa yake ya ubunge chini ya wakili wake Vitalisi Kimomogoro,rufaa hiyo iliyokuwa inasikilizwa mahakama kuu ya rufaa jijini Dar es salaam.

Ikumbukwe kuwa Mheshimiwa Lema alisimamishwa ubunge wake kupitia kesi iliyofunguliwa kwa madai kwamba wakati wa kampeni zake zilizoendeshwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitoa lugha isisiyotakiwa kwa mgombea wa CCM.

Thursday, December 20, 2012

UHABA WA MAJI MOROGORO
Bomba kubwa lenye kipenyo cha 16" sawa na 400mm limepasuka eneo la Msamvu stendi ya Dodoma karibu na kituo cha kusambaza umeme.Ingawa juhudi za kurejesha huduma ya maji kwa wakazi wa manispaa ya Morogoro zikiwa zinaendelea lakini changamoto nikwamba bomba hilo limekatiza barabara kuu ya kuelekea Dodoma ambayo ni ya lami,hivyo namna ya kuchimba inakuwa vigumu.


Akiongea kutokea eneo la tukio,kaimu Mhandisi wa usambazaji na matengenezo Bw.William Mbilizi alisema kuwa matengenezo hayo yanaweza kukamilika ndani ya siku 2.





Wednesday, December 12, 2012

SHORT COURSE ON FIRST AID.
INDUSTRIAL FIRST AID COURSE
OSHA has organized the above mentioned course for all nominate first aiders at workplaces or
any one in need of comprehensive introduction to first aid.
Objective of the course: To equip participants with adequate knowledge and practical skills in
dealing with health emergencies at workplaces.
Participants will be able to minimize the outcome of workplace accidents or exposures, along
with enhancing their workplace compliance to First Aid legal requirement.
Course contents:
 The First Aid provision as described in OHS act 2003.
 Contents/ uses of first aid kit.
 Medical emergencies(stroke, asthmatic and diabetic shock, epilepsy)
 Accidents and incidents.
 Treatment of an unconscious causality (CPR).
 Foreign bodies and eye injuries.
 Poisoning and allergic reactions.
 Burns and scalds.
 Fractures and dislocation.
 FIRST AID PRACTICAL.
The course will be conducted for three days from 18th – 20th December, 2012 at OSHA
headquarters office Training lounge.
Course fee is Tsh.200, 000/= per participants, this is only for tuition and refreshment during
course. NOTE: Breakfast and lunch will not be provided.
Training methodology: Instruction lectures, plenary session and practical demonstrations.
For more information and booking please contact the following;
Chief Executive Officer, P. O Box 519, Tel +255 22 2760548/2760579
Shaaban Mkindi – 0713 826849, Naanjela Msangi – 0715 424 020
Jamani tuchangamkie course hii.

Monday, December 3, 2012

MUHAS CONFERENCE



The Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS) announces its first scientific conference that will be organized with support from Sida and other development partners. We welcome all researchers, local and international, working in various areas of health to share their research findings with other stake holders in this conference.

The Conference will be held at Kunduchi Beach Hotel, Dar es Salaam on 2nd – 4th May, 2013.
Conference Theme: Health Research Towards Poverty Alleviation.
Under this theme, there are four sub-themes:
 A. Translating Health Research Findings into Policy and Practices
i. Best practices in prevention of communicable diseases (primary, secondary and tertiary)
ii. Best practices in prevention of non-communicable diseases (primary secondary and tertiary)
iii. Best practices from health systems and policy study findings (quality of health care: affordability, equity and accessibility)
iv. Innovations in health interventions
v. Complementary and Alternative approaches in healing practices (traditional medicine and nutraceuticals, probiotics)
 B. Progress in addressing Health Related Millennium Development Goals
i. MD Goal 4: Child morbidity and mortality
ii. MD Goal 5:  Maternal Health
iii. MD Goal 6:  HIV/AIDS
iv. MD Goal 7:  Environmental sustainability
v. Complementary and Alternative approaches in healing practices (traditional medicine and nutraceuticals, probiotics)
 C. Emerging Major Health Challenges
i. Lifestyle related diseases
ii. Various forms of violence and health outcomes.
iii. Injuries and Accidents
iv. Vaccines for preventable diseases (new development, coverage, preparedness, barriers and adverse reactions)
v. Conflicts and challenges
 D. Responding to the Crisis on Human Resource for Health
i. Training (pre and post service) to meet health needs
ii. Opportunities and challenges  in the allocation of human resource  for health
iii. Task shifting and task sharing initiatives; case studies and best practices and challenges

Note: In addition to vibrant scientific presentations, there will be exhibitions on new and innovative products, devices and equipment for diagnosis, management and prevention of diseases.

 Conference Secretariat
Directorate of Continuing Education and Professional Development
P.O.BOX 65001
Dar es Salaam
Tel: +255 22 2152431.
Committee Chairs, Steering Committee
Dr. G. Kwesigabo
Organizing Committee
Prof. S. Massawe.
Scientific Committee
Dr. D. Mloka

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...