Thursday, June 18, 2015

OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI YAENDELEA KUTOA ELIMU KWA UMMA.

Mkaguzi Fahd Masanja (Katikati) akitoa elimu kuhusu Ukaguzi wa Serikali Kuu kwa mmoja wa wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Kushoto ni Bw. Roy Mchomvu, Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta wa Ofis ya Taifa ya Ukaguzi.

Bibi Salma Pamui, Mkaguzi wa Idara ya Pensheni (aliyenyanyua mikono) akitoa elimu kuhusu uhakiki wa taarifa za wastaafu kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Idara ya Pensheni ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, ni Idara inayohakiki taarifa za wastaafu wote wa Serikali kabla ya kulipwa mafao yao.


Mkaguzi Mariam Chikwindo, mtaalam wa ukaguzi anayeshughulikia uhakiki wa matumizi sahihi ya fedha za umma akitoa elimu juu ya uwazi katika matumizi ya umma kwa wa wananchi waliotembelea Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Bi Sarah Reuben (Wapili kushoto) akizungumza na mmoja wa wananchi waliojitokeza kujua kazi zinazofanywa na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Wengine katika picha ni Wakaguzi, Bibi Tumaini Sorogo (Kushoto) na Bw. Fahdi Masanja (Watatu kushoto).

Bibi Tumaini Sorogo (Kushoto), Mkaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi akimsikiliza kwa makini mwananchi aliyekuwa akiuliza taarifa mbalimbali kuhusu wajibu na kazi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015. Maonesho haya yanaendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta, Bw. Roy Mchomvu akimsikiliza kwa makini mwananchi aliyetembelea Banda la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mkaguzi Salma Pamui (Kushoto) na Mkaguzi Mariam Chikwindo (Wapili kulia).

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali, Bi Sarah Reuben (Kushoto) akizungumza na mmoja wa wanahabari wakongwe nchini Tanzania, Bw. Pachal Mayala wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Mkaguzi Lenatus Leonard (Katikati) kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi akihojiwa kuhusu ufanisi wa ukaguzi kwa upande wa Serikali za Mitaa na Bw. Pachal Mayala wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwa mwaka 2015 yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
PICHA KUTOKA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI, MAKAO MAKUU.

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...