Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe duniani. |
Na Saidi Mkabakuli, Kigoma
Wakaguzi wa Miradi ya Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata fursa adhimu ya kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba iliyo kwenye Ziwa Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wakizungumza mara walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha bashasha waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe iliyo na umri zaidi ya miaka 100.
Mmoja wa wakaguzi hao Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana kuingia na kushuhudia mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini Tanzania.
“Nimefurahi sana kufika leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya ukongwe wake bado inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka mingi zaidi,” alisema.