Monday, November 3, 2014
Jaji Mstaafu Warioba adhalilishwa mdahalo wa Katiba
Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba akisaidiwa kutolewa katika vurugu |
Katika mazingira ya kutatanisha, siku ya Jumapili vurugu zimekatisha mdahalo uliokuwa ukiendelea kujadili mchakato wa katiba mpya ya Tanzania huku baadhi ya watu wakipigwa na kujeruhiwa.
Mdahalo huo uliokuwa ukitangazwa moja kwa moja kupitia redio na televisheni ulivurugika kutokana na kundi la vijana wapatao 20 kuanza kumzomea aliyekuwa mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipokuwa akiwasilisha mada yake.
Thursday, October 30, 2014
Wednesday, October 29, 2014
Tuesday, October 28, 2014
Monday, October 27, 2014
TATIZO LA MAJIKWA MJI WA MPANDA LATATULIWA, NI CHANZO CHA MAJI IKORONGO.
Na Mwandishi wetu, Katavi
Chanzo cha maji cha chemichemi ya Ikorongo ambacho ni cha asili kipo kilometa 13.2 kutoka Mpanda mjini, mkoani Katavi. Chanzo hiki cha maji kinazungukwa na miti na uoto wa asili unaolinda maji hayo yawe safi na salama kwa matumizi ya binadamu.
Mhandisi wa Maji wa Mkoa wa Katavi Magdalena Mkeremi anasema chanzo hiki cha maji ni chemichemi yenye maji masafi yasiyokauka hata wakati wa kiangazi.
Chanzo hiki kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni sita kwa siku.
Mradi wa maji wa Mji wa Mpanda ni wa gharama nafuu kwa sababu hautumii pampu ya aina yoyote bali maji husambazwa kwa njia ya mserereko (gravity).
Bomba kubwa la maji la inchi kumi limelazwa kutoka kwenye chanzo na kupelekwa Kazima kwenye tanki kubwa la ujazo wa lita milioni moja ambalo limejengwa eneo la kilometa 13 kutoka kwenye chanzo cha maji. Vile vile maji kutoka kwenye tanki hilo na kwenda mjini na katika mitaa au vijiji pia hutumia mserereko hivyo, kurahisisha gharama zake.
Subscribe to:
Posts (Atom)