Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa katika vyuo vinavyoendeshwa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2014/2015.
1. Kozi zinazotangazwa ni:
A. Kozi za ngazi ya Stashahada (Ordinary Diploma Programmes):
- Stashahada ya Afya ya Mazingira (Ordinary Diploma in Environmental Health Sciences)
- Stashahada ya Uzoeza viungo (Ordinary Diploma in Physiotherapy )
- Stashahada ya Teknologia ya Viungo Bandia vya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Dental Laboratory Technology)
- Stashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Ordinary Diploma in Health Laboratory Technology)
- Stashahada ya Optometria (Ordinary Diploma in Optometry)
- Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Ordinary Diploma in Clinical Medicine)
- Stashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Kinywa na Meno (Ordinary Diploma in Clinical Dentistry)
- Stashahada ya Uuguzi (Ordinary Diploma in Nursing)
B. Kozi za ngazi ya Cheti (Technician Certificate Programme)
- Astashahada ya Teknologia ya Maabara za Afya ya Binadamu (Technician Certificate in Health Laboratory Technology)
- Astashahada ya Utabibu wa Magonjwa ya Binadamu (Technician Certificate in Clinical Medicine)
- Astashahada ya Uuguzi (Technician Certificate in Nursing)
- Astashahada ya Teknologia ya Kutunza Kumbukumbu za Afya ya Binadamu (TechnicianCertificate in Health Record Technology)
- Astashahada ya Afya ya mazingira )Technician certificate in Environmental health Sciences)