Monday, March 24, 2014

MVUA ZALETA MAAFA BUKOBA.

L
Usiku wa kuamkia leo mji wa Bukoba umepata mvua ya kutosha iliyosababisha migomba na mazao mengine kuharibika vibaya sana. Hali hii imesababisha hata na baadhi ya makazi kuhezuliwa. Camera yetu imetembelea kata ya Bakoba katika mitaa ya Bunena na kujionea hali ilivyo baada ya kuanguka migomba na wananchi wakiendelea kukata baadhi iliyoangukia mazao mengine na baadhi ya maeneo ya Kashenye.


ORODHA YA WATUMISHI WA AFYA WATAKAOFANYA MITIHANI YA KUJIENDELEZA – MWAKA 2014

BOFYA HAPA.

TANGAZO LA KAZI UTUMISHI (TANZANIA TEA BOARD) 21 MARCH 2014.

Friday, March 21, 2014

ROBO FAINALI YA UEFA, MAN U vs BAYERN.

QUARTER-FINALS-1/2 AND 8/9 APRIL


BarcelonaBarcelona(ESP)
v
AtléticoAtlético(ESP)

Real MadridReal Madrid(ESP)
v
DortmundDortmund(GER)

ParisParis(FRA)
v
ChelseaChelsea(ENG)

Man. UnitedMan. United(ENG)
v
BayernBayern(GER)

JOB VACANCY MANAGING DIRECTOR - TPDC.

SERIKALI KUFUFUA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE.

Timu ya wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Tume ya Mipango wakitazama bidhaa zilizokuwa zikitengenezwa na kiwanda cha matairi cha General Tyre. Serikali ina mpango wa kufufua kiwanda hicho ambacho kilisimama uzalishaji tangu mwaka 2007.
Timu ya wakaguzi wa miradi wa maendeleo wakiangalia mitambo ya kiwanda cha matairi cha General Tyre jijini Arusha

Short Course in Traditional Medicine Development - MUHAS.

Thursday, March 20, 2014

NEEMA KWA WANAMTWARA, UWANJA WA NDEGE KUBORESHWA.

Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (aliyevaa fulana nyeusi) akihoji uimara wa sehemu ya kutulia ndege wakati walipofanya ziara ya kujionea maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Katika kukabiliana na kasi ya maendeleo ya ukuaji wa uwekezaji katika maeneo ya viwanda vikubwa na biashara za huduma mkoani Mtwara, Serikali imesema kuwa kuna haja ya kuuimarisha Uwanja wa Ndege wa Mtwara ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa watumiaji wa uwanja huo, hasa kufuatia kugundulika kwa gesi mkoani humo,
Hayo yamebainishwa mmoja wa viongozi wa timu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri  wakati ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja wa huo.
Bibi Mwanri alisema kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini na mikakati mbalimbali itakayopelekea kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara ili kuweza kuhudumia uwekezaji mkubwa unaofanywa na makampuni mbali mbali ya ndani na nje ya nchi mkoani humo. Aliongeza:
“Tathmini ya awali inaonesha kuwa miradi mingi ipo mkoani Mtwara kufuatia kugundulika kwa gesi hivyo kuna haja ya dhati ya kuuimarisha uwanja wa ndege wa Mtwara kwa lengo la kutoa huduma za uhakika wakati huu wa mfumuko wa kiuchumi mkoani Mtwara,” alisema Bibi Mwanri.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara, Mhandisi Mugasa Mlondo akitoa maelezo juu uimara na ubora wa uwanja wake wakati Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara kwa ajili ya kujionea maendeleo ya uwanja huo.

NAFASI ZA KAZI UTUMISHI, DEADLINE APRILI, 04.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...