Mamia ya waislam wamefanya maandamano katika mji mkuu wa wa Mauritania Nouakchott, baada ya kuenea kwa taarifa kuwa Koran imechanwa msikitini.
Imam ameripoti kuwa watu wanne waliokuwa wamefunika nyuso zao waliingia msikitini , wakachana nakala za Koran na kuzitupa chooni.
Mauritania ni taifa la kiislam , likiwa na idadi ndogo ya wakristo.Polisi walifyatua mabomu ya kutolea machozi kutawanya umati wa watu waliokuwa na jazba, na mtu mmoja aliuawa, duru za polisi zilieleza.
Imekuwa mshirika muhimu wa nchi za magharibi katika kampeni dhidi ya al-Qaeda na makundi mengine ya wanamgambo yanayoendesha harakati katika kanda hiyo .
Mwandishi wa habari Hamdi Mohamed El Hacen aliyeko mjini Nouakchott anasema waandamanaji walichoma vizuizi na maduka mengi na masoko yalifungwa jana siku nzima.
Mamia ya waandamanaji walikusanyika kati kati mwa mji mkuu na nje ya msikiti wakipaza sauti "Mungu ni mkuu" wakidai wahusika wakamatwe na kuhukumiwa kifo kwa madai ya kukufuru uislam, alisema.
Source: BBC