UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU
TANZANIA
(TFF)
14/08/2013
1. Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawatangazia
wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa TFF utafanyika tarehe
20/10/2013 jijini Dar es salaam. Wale wote wanaopenda kuwania nafasi za
uongozi wa TFF wanataarifiwa kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF
zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe 20 Agosti 2013
katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF (Idara ya Fedha), kuanzia saa 03:00
asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni saa 10:00
Alasiri tarehe 20 Agosti 2013.
2. Nafasi
zinazotangazwa kugombewa ni:
(i)
Rais wa TFF.
(ii)
Makamu wa Rais wa TFF.
(iii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF, nafasi kumi na tatu (13).
3. Mtu
yeyote anayeomba nafasi ya uongozi katika TFF lazima atimize masharti
yafuatayo:
(i)
Awe Raia wa Tanzania.
(ii)
Awe na kiwango cha elimu
kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari.
(iii)
Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira
wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)
Asiwe na hatia yoyote ya kosa la
jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)
Awe na umri wa angalau miaka 25.
(vi)
Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira
wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa
Miguu katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza.
(vii)
Awe mwadilifu, mwaminifu na mwenye
uwezo wa kutekeleza majukumu, wajibu na malengo ya TFF kwa weledi.
(viii) Mtu
anayegombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa TFF lazima awe na
kiwango cha Elimu kisichopungua Shahada ya Chuo Kikuu na awe na uwezo na
haiba ya kuwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.
4. Ada za Fomu
za maombi ya uongozi ni hizi zifuatazo:
(i)
Rais wa TFF; Shillingi Laki Tano
(Tshs. 500,000/=).
(ii)
Makamu wa Rais wa TFF; Shillingi
Laki Tatu (Tshs. 300,000/=).
(iii)
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
5. Kwa wale
ambao walilipia fomu za kugombea katika mchakato uliofutwa na ambao
wanakusudia kugombea nafasi zile zile walizozilipia, hawatalipia tena
ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati
wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.