Tuesday, May 14, 2013

ONYO KWA WANAOUZA DAWA NA VIPODOZI KWENYE MABASI & TRENI.

 MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
                                                            TAARIFA KWA UMMA
ONYO KWA WANAOUZA DAWA NA VIPODOZI KWENYE MABASI
Kumekuwa na tabia kwa wafanyabiashara wadogo wadogo kuuza bidhaa aina ya dawa na vipodozi kwenye vyombo vya usafiri hasa treni na mabasi ya abiria. Uuzaji wa bidhaa hizi kwenye vyombo vya usafiri ni kinyume na Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura 219 ya mwaka 2003. Sheria hii inapiga marufuku kufanya biashara kwenye maeneo ambayo hayajasajiliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri.


JOB VACANCIES - DAWASCO.


DAWASCO is a Public Corporation which was established to provide Water and Sewerage Services to the City of Dar Es Salaam and some parts of Coast Region. Currently it has vacancies in its Finance and Commercial Departments which has to be filled immediately.


Applications are now invited from suitable qualified candidates to fill in the following Posts:-    




Call for Papers Mzumbe University - Submission Deadline : J une 14 th , 20 1 3


Journal of Policy and Leadership (JPL), ISSN 1821–8318
Journal of Policy and Leadership (JPL) is an academic journal from the Centre of Policy and
Leadership, School of Public Administration and Management, Mzumbe University aiming to involve scholars not only from Tanzanian Universities, but also from all international and professional communities. The Journal accepts original theoretical and empirical research articles, reviewed articles and books focusing on any aspect of leadership, public policy and administration in Africa as well as articles based on experience outside Africa but which provide useful comparative lessons.
To continue and for more information,click the following link:
http://main.mzumbe.ac.tz/documents/Journal_of_Policy_and_Leadership.pdf

EMPLOYMENT OPPORTUNITY- MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO.

 
MUSLIM UNIVERSITY OF MOROGORO
P.O. BOX 1031 Morogoro, Tanzania
Tel: +255 23 2600256 Fax: +255 23 2600286
E-mail address:mum@mum.ac.tz
Website: www.mum.ac.t
EMPLOYMENT OPPORTUNITY
The Muslim University of Morogoro is a private institution of higher learning established
in October 2004 by the Muslim Development Foundation. It was established by a
Charter on 23rd October 2004 and it is fully registered by Tanzania Commission for
Universities.
The Muslim University of Morogoro would like to recruit a qualified, self– motivated, experienced and qualified person to fill the following vacant position:
 
JOB TITLE: Examination Officer
Applicants should posses the following criteria.
 

SHORT COURSE - MUHIMBILI (25-29 JUNE,2013).


Organization of knowledge: Classification, Cataloguing & Subject Analysis (25-29 June 2013)
Continuing Education & Professional Development
2013 Certificate Short Course

Date: 25th - 29th June 2013                                         

Venue: Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS)

Course Fee for Tanzanians: 350,000 TShs   

Course Fee for Non-Tanzanians:US$ 300

Overall Course objectives: To equip the participants with the relevant skills and knowledge in library cataloguing and classification and subject analysis

Who Should Attend? Professionals involved in information management, institutional management, librarians, lecturers ,project administrators and any other professional who has a use for library cataloguing and classification and subject analysis in their work.

Course Main Topics:
·         Specifically the course will cover:

·         Descriptive cataloguing of library materials using AACR2 rules

·         Subjects analysis and formulation of subject headings.

·         Application of Library of Congress and Dewey Decimal Classification schemes.

·         CIP Cataloguing and LC online cataloguing

Training Format: Training over 5 consecutive days, Face to face in a group setting and practical sessions for online cataloguing tools, Attendance on all 5 days is required for certificate of completion

For further information about the workshop  and workshop registration, please contact the following:
Kesia Rad
library@muhas.ac.tz

Also copy to:
Mr William Mviombo
Email: mviombo@yahoo.com,
mviombojulius@gmail.com
+255713236649
Mr Christom Mwambungu:
cmwambungu2010@yahoo.com
+255713312413

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI MHESHIMIWA SAID AMOUR ARFI (MB).

 

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHESHIMIWA SAID AMOUR ARFI (MB), WIZARA YA UJENZI, KUHUSU MAPITIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014 (Inatolewa chini ya Kanuni ya 99(9) toleo la mwaka 2013)


1.0      UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, jukumu la msingi la Wizara hii ni kusimamia kukamilifu tasnia ya ujenzi kwa ukamilifu wake ili kutoa matokeo bora na kuchochea uchumi wa nchi yetu na kuwaletea maendelo watu wetu na kupunguza umasikini kwa kuwa na miundombinu yenye kukidhi viwango, ubora na Usalama.
2.0      MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI 2012/2013
Mheshimiwa Spika, ukusanyaji wa vyanzo vya mapato katika idara na vitengo vya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2012/13 ulivuka lengo la mwaka hadi kufikia Februari 2013 walikusanya zaidi ya mara mbili ya lengo la makusanyo kwa mwaka. Halikadhalika mfuko wa Barabara ulikusanya takriban asilimia 70 hadi februari 2013 ni dhahiri mfuko wa barabara nao utafikia lengo uliokusudia kwa mwaka 2012/13 na kuvuka lengo, haya si mafanikio haba, hata hivyo hayajakidhi wala kupunguza changamoto za Wizara hii.
Mheshimiwa Spika, matumizi ya kawaida na maendeleo, wizara imeendelea kupokea fedha kwa mtiririko unaoridhisha, matumizi ya kawaida  hadi februari 2013 ilipokea 69% ya fedha za matumizi na 100% kwa miradi ya maendeleo kwa fedha za ndani zilikuwa zimepokelewa.
Mheshimiwa Spika, yapo matukio kadhaa yaliyotokea ambayo Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Maelezo ya kina na kutosheleza na hatua zilizochukuliwa ili kuzuia hali hii isijirudie tena na kuleta maafa kwa watanzania. Kambi Rasmi ya Upinzani inatambua majukumu ya Wizara hii pamoja na kuzisimamia taasisi zilizopo chini ya Wizara hii ikiwemo Baraza la Ujenzi (NCC), Bodi ya Usajili wa Wahandisi(ERB), Bodi ya Usajili wa Wabunifu majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQSRB), Pia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na vyombo hivi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu za miundo yake.
Mheshimiwa Spika, yamekuwepo matukio ya kujirudia ya kuanguka kwa majengo ya magorofa yaliyokamilika na yanayoendelea kujengwa katika jiji la Dar es Salaam na tukio la hivi karibuni jengo lililokuwa linaendelea kujengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam, mtaa wa Indira Ghandi na kupoteza maisha ya Watanzania kadhaa, Kambi Rasmi ya Upinzani inatoa pole kwa wale wote waliopoteza  ndugu na marafiki zao katika tukio hilo Mwenyezi Mungu awapumzishe kwa amani. Aidha,tukio la kuanguka kwa ukuta katika kituo cha Mabasi Ubungo na kuharibu magari na mali za watanzania ambao walifika katika kituo kikuu cha mabasi cha Ubungo kwa kujipatia huduma. Kambi Rasmi ya Upinzani inasikitishwa kwa tukio hilo ambalo lingeweza kuzuilika iwapo mkandarasi angezingatia kanuni za usalama. Tunapenda kuwapa pole watanzania wenzetu waliokumbwa na mkasa huo.
Mheshimiwa Spika, pole na kufarijiana pekee haitoshi bado tunajiuliza kama nchi ni lini viongozi wetu wataheshimu, kuwajibika na kutekeleza majukumu yao na kuwa na ujasiri wa kutafuta mbinu za kutatua matatizo pindi tunapokutana na mambo magumu katika utendaji wetu na si kukimbia  matatizo kwa kujificha  chini ya migongo ya watendaji wengine na kutowajibika na uozo unaotokea katika wizara tunazozisimamia na tukisubiri kusifiwa kwa mazuri yanayofanywa na watendaji haohao na kukwepa lawama kwa mambo ya ovyo.
Mheshimiwa Spika, wakati waziri anawasilisha hotuba yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha uliopita alisema kuwa, naomba kunukuu “Bodi itafanya ukaguzi wa kina katika taasisi za elimu ya juu zinazofundisha uhandisi ili kubaini kama vyuo hivyo vina sifa stahiki za kufundisha wahandisi na iwapo wahadhiri wanaofundisha wahandisi wamesajiliwa na Bodi” (Hotuba ya bajeti ya waziri wa ujenzi 2012/2013, uk 162).

Kuendelea bofya Read More


Monday, May 13, 2013

ROLI LAPINDUKA MBEYA,LAUA 1 NA 3 WAJERUHIWA.

Kumetokea ajali ya Lori lenye namba za usajiri T.376 BXD ktk mteremko wa mlima Mbalizi Wilayani Rungwe,Mkoa wa Mbeya yaua mtu mmoja (1) papo hapo na wengine 3 kujeruhiwa vibaya.
Taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo tutawaletea kadiri tutakavyokuwa tunazipata.

LADY JAY DEE AFIKISHWA MAHAKAMANI NA CLOUDS FM.


MWANAMUZIKI Mahiri wa Bongo Fleva, Judith Wambura 'Lady Jaydee' leo alifika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kufunguliwa kesi ya madai katika mahakama hiyo. 
Katika hati ya madai hayo, mwanamuziki huyo anashitakiwa na viongozi wa Clouds Media Group ambao ni Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. ...
Mkurugenzi wa Clouds FM bwana Ruge Mutahaba.
Tuhuma za kesi hiyo zinatarajiwa kusomwa mahakamani hapo na Hakimu, Athuman Nyamrani Mei 27 mwaka huu. 
Jaydee aliwasili mahakamani hapo akiwa na mumewe Gadner G. Habash mishale ya saa 6 mchana na kuongoza moja kwa moja chumba cha makarani wa mahakama hiyo ambao aliwakabidhi hati ya mashitaka hayo.

WANAUME 2 WATAKA WARUHUSIWE KUJINYONGA.

Huyu ni Marehemu Tony Nicklinson naye aliwahi kutaka mahakama imruhusu auawe kwa usaidizi wa daktari kwa sababu ya ulemavu wake
Wanaume wawili wenye ulemavu mbaya zaidi wanakwenda mahakamani kukata rufaa katika kesi inayoonekana kuwa moja ya kesi inayotaka mageuzi makubwa ikitaka kubadilisha sheria za serikali kuhusu haki ya mtu kufa.
Mmoja wa watu hao, Pail Lamb amekuwa na ulemavu mbaya kwa miaka mingi pamoja na kupitia uchungu mwingi, hawezi kujitoa uhai wake na anataka madaktari waruhusiwe kumuua bila ya kukabiliwa na kosa la mauaji baadaye.
Mwanamume mwingine anayejulikana kama Martin, anataka uamuzi utakaowaruhusu madaktari wamsaidie kujiua ingawa waweze kulindwa kutokana na sheria za kuweza kuwashtaki kwa kufanya kitendo cha mauaji.
Wakosoaji wanasema kuwa ikiwa mahakama itaruhusu wawili hao wajiue, itakuwa na athari kubwa kwa watu wazee na wenye ulemavu kutaka kujinyonga ili kuzuia kuwahangaisha jamaa zao kuwahudumia.

Source:BBC

KATUNI NA MECHI YA SIMBA vs YANGA MEI 18.


LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...