Tuesday, November 6, 2012

HATARI! HATARI! HATARI!
Hii ni hatari kwa wakazi wa Manispaa ya Morogoro wanaonunua maji kutoka kwenye magari yanayouza maji mitaani.Magari haya badala ya kununua maji katika vioski vya kuuzia maji vilivyo mjini yanaenda eneo la Mindu darajani na kuchota maji yasiyo tibiwa na kwenda kuwauzia wananchi.
Kibaya zaidi nikwamba magari hayo yameandikwa majisafi hivyo wananchi wanayaamini kumbe mambo ni tofauti.
Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa MORUWASA inasambaza maji yasiyosafi na salama baada ya kutumia maji kutoka kwenye magari hayo yanayowadanganya watu kuwa wamenunua maji kutoka MORUWASA.Mojawapo ni gari T 706 AAF lililoandikwa majisafi,naomba wahusika wafatilie suala hili kwa karibu ili kunusuru afya za wananchi.
KUPASUKA BOMBA.
Bomba kubwa linalotoa maji bwawa la Mindu kupeleka sehemu ya kutibia maji Mafiga lenye kipenyo cha inchi 24 (24") sawa na milimeta 600 (600mm) limepasuka sehemu mbili tofauti.Bomba hili ndo linalosambaza maji mjini Morogoro zaidi ya asilimia 75.
Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira inaendelea na juhudi za kulitengeneza bomba hilo kama inavyoonekana kwenye picha ili huduma ya maji ilejee haraka iwezekanavyo.
Matengenezo hayo yanatarajiwa kukamilika kabla ya yaa 12 jioni.
UZEMBE KAZINI.
Hapa ni mchezo wa makida unachezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro katika suala zima la utupaji wa taka ngumu.Jambo la kusikitisha nikwamba magari yanamwaga taka hadi barabarani baada ya kujizibia barabara ya kuingia dampo.
Swali langu ni,je,muhusika wa taka ngumu huwa anatembelea dampo hili? Na kama anatembelea ni  hatua gani kazichukua katika kutatua tatizo hili?
Jambo jingine la kusikitisha nikwamba magari haya ya takangumu yameanza kumwaga taka hizo nje ya uzio kwa uzunguka uzio huo na kuzichoma moto nje ya dampo.
Jamani,tujali afya za wananchi popote tulipo na tujenge utamaduni wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira.
HALI SI NZURI.
Jopo la wamahabari wa vyombo vya habari mbali mbali walitembelea vyanzo vya maji vya Manispaa ya Morogoro na kujionea hali halisi ya maji katika vyanzo hivyo.
Hali ya kusikitisha ilikutwa katika Bwawa la Mindu ambako maji yanazidi kukauka na kusababisha upungufu wa maji kuzidi kuongezeka.
Wakazi wote Morogoro na Tanzania kwa ujumla tuna jukumu la kutunza mazingira ili hata mvua ziweze kunyesha za kutosha.
VIWANDA VYA MOROGORO VYATELEKEZWA.
Zilikuwa ni juhudi za Mwl.J.K.Nyerere za kujenga viwanda hasa eneo la Morogoro lakini cha kushangaza viwanda karibu vyote vimekufa hasa baada ya kubinafsishwa.
Mpaka sasa viwanda ambavyo vinahali mbaya ni kiwanda cha viatu cha MOROSHOE na kiwanda cha bidhaa zinazotokana na ngozi LEATHER GOODS.Viwanda hivi havifanyi kazi zaidi ya kuanza kuporomoka na kuanguka.
Wito wangu kwa serikali ni kuvifufua viwanda hivi ili vifanye kazi kama vilivyo kusudiwa ikizingatiwa kuwa ni fedha za kodi za wananchi ndo zilizotumika kujengea viwanda hivi.
FAHARI YA MOROGORO ISIYOTHAMINIWA.
Mji wa Morogoro umezungukwa na milima ya Uluguru ambayo ina vivutio mbali mbali ikiwa ni pamoja na wanyama adimu aina ya MBEGA.Milima hii ni tegemeo kubwa la vyanzo vya maji katika mikoa ya Morogoro,Pwani na Dar es salaam.Bwawa la Mindu ambalo linategemewa na wakazi wa Manispaa ya Morogoro linaloundwa na mito mitano yote inaanzia katika safu za milima ya Uluguru.
Milima hii kipindi cha miaka ya sabini maji yalikuwa yakitiririka milimani lakini kama inavyoonekana watu wameivamia milima hii na kuendesha shughuri mbali mbali kama kilimo na uwindaji wa wanyama.Kutokana na uharibifu huo kwa sasa hali ya maji inazidi kuwa mbaya.
Jamani tushirikiane wote katika kurudisha hali ya milima hii ya Uluguru.
AFYA
Sehemu nyingi za kazi afya za watendaji wa kazi hazijaliwi.Kinachofanyika hapo ni mwajiri kuona kazi yake imekamilika lakini mazingira ya kukamilika kwa kazi hiyo hayafatilii na kuyafanyia kazi.Kutokana na Sheria ya Afya na Usalama kazini (The Occupational Health and Safety Act,2003) kifungu namba 62,wafanyakazi wote wanatakiwa kupewa vitendea kazi na vifaa vya kujikinga na madhara ya kazi wanazozifanya...
Expand this post »
UKATAJI MITI OVYO.
Hili ni kanisa mojawapo hapa Manispaa ya Morogoro ambalo linatumia magogo kama viti vya kukalia waumini wake wawapo kanisani.Ili kuwa na matumizi endelevu ya rasilimali,bora zingepasuriwa mbao harafu tukatengeneza mabenchi kuliko kukata magogo kama inavyoonekana.
Hili ni kanisa la SAUTI YA UPONYAJI la NABII JOSHUA lililo Kihonda Viwandani karibu na Kiwanda cha Ngozi.
UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
Matumizi ya nishati ya misitu katika viwanda vyetu hata Morogoro yanazidi kuongezeka kiasi kwamba viwanda vingine vinatumia kuni kuendeshea mitambo ili kukwepa gharama za umeme.Kiwanda kimojawapo kinachotumia  kuni kuendeshea mitambo yake ni 21st Century Textiles Ltd.
Haya ni magogo yaliyorundikwa kusubiria kutumika.Jamani,kutengeneza msitu inaweza kutuchukua muda si chini ya miaka kumi lakini ufyekaji unaweza kufanyika ndani ya siku kadhaa tu.Kibaya zaidi hawa wanaokata miti ukiwauliza wamepanda mingapi utaambiwa hawajapanda mti hata mmoja.
Watanzania tuamke,tutunze mazingira yetu ili hata vizazi vijavyo vikute hizi rasilimali tulizonazo.
INDUSTRIAL WASTE WATER MANAGEMENT.
Morogoro ni mji mmojawapo ambao Baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere aliufanya uwe wa viwanda vingi ambavyo vilikuwa vya Tumbaku,Ngozi,Maturubai,Nguo,Magunia,Viatu n.k.Baada ya ujenzi wa viwanda hivi palijengwa mabwawa ya majitaka ya viwandani mahususi kwa kuhudumia hasa Kiwanda cha Selamic,Moroshoe na Canvas.Mabwawa hayo  yalikuwa chini ya miliki ya TLAI,lakini baada ya viwanda kubinafsishwa mabwawa hayo yakawa hayana mwangalizi kama inavyoonekana.
Ombi langu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,iangalie uwezekano wa kuyakarabati mabwawa haya ili kunusuru afya za wananchi.
4 photos

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...