Tuesday, November 6, 2012

DUMPING SITE MOROGORO MUNICIPAL.
Hii ndo hali halisi ya dampo la Manispaa ya Morogoro ambalo halijaliwi na wala halifanyi kazi yake kama ilivyokusudiwa .Taka ngumu zinamwagwa hadi getini kiasi kwamba hata gari la taka ngumu haliwezi kuingia kumwaga taka.Kibaya zaidi taka hizo zinachomwa hapo hapo zilipo mpaka moto unatoka nje ya fensi ya dampo hilo kama inavyoonekana.Swali langu kwa Halmashauri ya manispaa ya Morogoro Idara ya afya ,je,hali hii wanaijua? Kama wanaijua hatua gani zimechukuliwa.Badala ya kuwa contolled tipping inakuwa crude dumping.Tafakari,chukua hatua.
UKAME! UKAME! UKAME! UKAME!
Hali ya maji Morogoro inazidi kuwa mbaya baada ya Bwawa la Mindu kupungua kina cha maji kwa kasi baada ya ukame kuendelea kukausha maji.Hii yote inatokana na uchafuzi wa mazingira.Hivi ndivyo bwawa la Mindu linavyoonekana.
MATUNDA.
Morogoro inasifika kwa kuwa na matunda aina mbali mbali ya kutosha ambayo yanapatikana maeneo tofauti ya mkoa wa Morogoro.
Changamoto kubwa ninayoiona hapa ni utunzaji wa matunda hayo yanayoletwa mjini.Yanamwagwa tu chini bila kujali usalama wake swala ambalo linaweza kuleta madhara kiafya kwa walaji.Wafanya biashara wa matunda wawe wanafatiliwa kwa ukaribu ili kuweza kuwadhibiti kutoharibu ubora wa matuda hayo.Wafanyabiashara hawa wamekutwa wamemwaga matunda chini eneo la Sume Mwembesongo.
BARAZA LA WAFANYAKAZI.
Hili ni baraza la wafanyakazi la Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Morogoro (MORUWASA) lenye jumla ya wajumbe 42.Baraza hili lina majukumu mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwatetea wafanyakazi na kupitisha makisio ya bajeti za Mamlaka.
Baraza hili lilizinduliwa rasmi tarehe 13/06/2012 na Mwenyekiti Taifa wa Chama cha wafanya kazi wa serikali kuu na Afya (TUGHE) Dr.Mrutu.
HALI YA MAJI MOROGORO.
Wakazi wa Manispaa ya Morogoro wanategemea chanzo cha maji cha bwawa la Mindu kwa zaidi ya asilimia 70 (70%) .

 Bwawa hili lilianza kujengwa mwaka 1980 na kukamilika na kufunguliwa tarehe 09 Mei,1985 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania- Mwl.Julius Kambarage Nyerere.

Bwawa hili lilikuwa na uwezo wa kutunza maji galoni bilioni 12 sawa na milioni 12 za meta za ujazo (12 million metre cube).Hata hivyo uwezo wake umeshapungua kutokana na kujaa tope linalotokana na shughuri mbali mbali za kijamii.
UKUSANYAJI NA USAFIRISHAJI TAKANGUMU MOROGORO.
Halmashauri ya Manispaa Morogoro katika kujitahidi kudhibiti uchafuzi wa mazingira imeanzisha sheria ndogo ya kutoa adhabu kwa kulipa Tsh.50,000/= kwa kila atakayekamatwa anachafua mazingira.Kwa kiasi firani  sheria hii imesaidia kupungua uchafuzi wa mazingira.
Hata hivyo,Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro imenunua magari 3 kwa ajili ya kusaidia ukusanyaji...
Expand this post »
UKUSANYAJI,USAFIRISHAJI NA UTUPAJI WA MAJITAKA MOROGORO.
Katika kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa majitaka katika Manispaa ya Morogoro,MORUWASA inamiliki mabwawa ya majitaka ambayo yanatumika  kwa suala zima la utibuji majitaka yote yanayokusanywa kutoka katka maeneo mbali mbali ya Manispaa.
Hatahivyo,changamoto kubwa katika ukusanyaji wa majitaka ni kutokana na kutoenea katika maeneo makubwa ya Manispaa kwani ni 13% ya wateja wenye majisafi ndo wana huduma hii ya mtandao wa majitaka.
Hii ni kutokana na maeneo mengi kuwa na miinuko na mabonde,gharama za  kugharamia uunganishwaji.
UKUSANYAJI WA TAKA NGUMU MOROGORO.
Katika Manispaa ya Morogoro suala la ukusanyaji taka ngumu naona limechukua sura mpya baada ya kuibuka biashara ya chupa za plastiki na kusaidia usafishaji wa Manispaa kuwa rahisi.Ni dhahili kuwa biashara hii inasaidia sana katika usafishaji.Hawa ni baadhi ya wakazi wa wakazi wa Manispaa ya Morogoro kama walivyokutwa wakisafirisha taka ngumu katika eneo la Mtawala.
UCHAFUZI WA MAZINGIRA MOROGORO.
Huu ni uchafuzi wa mazingira unaoendelea katika Manispaa ya Morogoro ambao unafanywa na uchomaji wa taka ngumu katika dampo la taka ngumu lililoko Kihonda Viwandani.Badala ya kufukia taka ngumu hizo kama inavyotakiwa (Controlled tipping) licha ya eneo hilo kuruhusu,kinachofanyika ni kzichoma taka ngumu hizo na kusababisha uchafuzi wa hewa (Air pollution)

Monday, October 8, 2012

MORUWASA katika kutekeleza majuku ya ke ya kuwapatia maji safi na salama wakazi wa Manispaa ya Morogoro,hii sehemu ya machujio ya kutibu maji katika kituo cha kutibu maji Mafiga.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...