Tuesday, August 22, 2017

ZAMBI APIGIA DEBE UWEZESHAJI WA KILIMO CHA UFUTA NA MIHOGO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi (hayupo pichani) wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Lindi.

Na Mwandishi wetu, Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kukopesha wakulima wa mazao ya ufuta na mihogo ili waweze kulima kilimo cha kisasa na cha kibiashara hasa kwa wakulima wadogo wadogo wa mkoani humo.
Bw. Zambi alitoa wito huo wakati wa mkutano wa Wadau wa Korosho na Ufuta Mkoa wa Lindi uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Bw. Zambi alisema kuwa mkoa wa Lindi ni mkoa uliojaaliwa katika kuzalisha mazao ya ufuta na mihogo lakini changamoto kubwa ni mtaji wa kulima kibiashara ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.
“Wakulima wa mkoa wa Lindi wapo tayari kushiriki katika kuleta mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara lakini kwa sasa suala la mtaji wa kilimo cha kibiashara ni changamoto kubwa,” alisema Bw. Zambi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga alisema kuwa Benki ya kilimo ipo tayari kutoa mikopo kwa wakulima wadogo wadogo waliokuwa kwenye vikundi ili waweze kukopeshwa.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...