Tuesday, February 28, 2017

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa afungua mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma leo Ikulu- Jijini Dar es Salaam

 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akitoa hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam mapema leo. Mkutano huo uliandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Takwimu zinazoonesha hali ya uzazi salama Nchini Tanzania




Monday, February 27, 2017

WANACHAMA PSPF SASA RASMI KUPATA MIKOPO KUPITIA BENKI YA CRDB

 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.

HABARI PICHA - WAZIRI MKUU MSTAAFU PINDA AZINDUA KONGAMANO LA WADAU WA SUA NA KUTEMBELEA BANDA LA TADB

Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Deogratias Lutatora (Kushoto) na Mkuu wa Chuo cha Kilimo, Prof. Susan Nchimbi-Msolla (Wapili Kushoto) wakimuongoza Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Mwenye tai nyekundu) kufungua Kongamano la Wadau la SUA. Kushoto kwa Mhe. Pinda ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe.

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Wadau la SUA mara baada ya kufungua Kongamano hilo. Wengine waliokaa ni  Kushoto kwa Mhe. Pinda ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Kaimu Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA), Prof. Deogratias Lutatora (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe (Kulia).

Friday, February 17, 2017

RED CROSS YAKABIDHI KADI ZA UANACHAMA IDARA YA MAAFA

Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw. Mwadini Jecha (katikati) akiweka saini kitabu cha wageni Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea Idara hiyo na kukabidhi Kadi za Uanachama kwa Idara  hiyo, tarehe 16 Februari, 2017.

Wednesday, February 15, 2017

ACACIA, UDSM INKS MOU TO IMPROVE ENGINEERING INDUSTRY IN THE COUNTRY


Vice Chancellor of the University of Dar es Salaam, Professor Rwekaza Mukandala, (L), and Deo Mwanyika, (R) , who is Acacia Vice President (Corporate Affairs), exchange documents after they had signed at the University’s Mlimani campus in Dar es Salaam late on Tuesday. The University of Dar es Salaam (UDSM) has signed a renewed Memorandum of Understanding (MoU) with Acacia Mining that would support 52 students and staff in various areas hence to improve quality of engineering sector. Right is Acacia's Chief Advisor, Learning and Training, Jannet Reuben Lekashingo, and UDSM's Acting Secretary to Council and Corporate Counsel 
who is also, the Intellectual Property Manager,
Dr. Saudin Mwakaje.
 K-VIS BLOG/Khalfan Said

<!--[if gte mso 9]>

JOB VACANCIES - SUA

Sunday, February 12, 2017

JOB VACANCIES - SUZA

LIST OF SUCCESSFUL LOAN APPELLANTS 2016/2017

The Higher Education Students’ Loans Board wishes to announce successful loan appellants. List of students is attached below.
Details of the loan allocations will be available in their respective institutions by end of 13th February, 2017.
Issued by:
EXECUTIVE DIRECTOR
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
11th February, 2017.

Saturday, February 11, 2017

HABARI PICHA: KUHAMIA KWA SERIKALI MAKAO MAKUU DODOMA

OFISI ZA MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA NDANI YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM)
Serikali katika kutekeleza agizo la Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. John P. Magufuri kuwa ofisi zote za serikali zinatakiwa kuhamia Dodoma, na kufuatia Ofisi ya Waziri Mkuu kuwa ilishahamia Dodoma, Wizara zingine zimeshahamia Dodoma ikiwa ni pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora ambazo ofisi zao ziko ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Friday, February 10, 2017

UTEUZI WA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA PAMOJA NA KAMISHNA MKUU WA UHAMIAJI


TADB YAANZA KUTEKELEZA MKATABA WA USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA MOROCCO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Maendeleo ya ya Kilimo Tanzania Bw. Francis Assenga (Katikati) Akiva Kwenye Kupamba Ukuta ya Pamoja baada ya viongozi wa Mikopo Agricole baada Tamwil El Fellah Wakati walipokagua Miradi mbalimbali ya Kilimo baada ya ufugaji katika vijiji Vya MJI wa Khemisset nchini Morocco jana. Kulia Kabisa nai Bw. Albert Ngusaru ambaye Mkurugenzi nai wa wa Hazina baada ya Utafutaji Fedha TADB.


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) has ilianza kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Ushirikiano wa saini kati ya Serikali ya Tanzania na Morocco wakati wa ziara ya Mfalme wa ziara Morocco Mtume Mohammed VI wa Tanzania kwa mwaliko wa jeshi Rais wa Jamhuri ya Tanzania , Mhe. Dk John Magufuli Bia katika Oktoba 2016.

Wednesday, February 8, 2017

WAZIRI MHAGAMA: VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI YETU SOTE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia wakati wa kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi Bungeni Dodoma.

Na mwandishi wetu.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mapambano ya kukabiliana na tatizo la Dawa za Kulevya ni jukumu la kila mwananchi na wala sio suala la kuiachia Serikali peke yake.

Ameyasema hayo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia juu ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya UKIMWI na Dawa za Kulevya iliyoibua maswali kwa Serikali kuendelea kupambana na wanaoshiriki katika biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.


Monday, February 6, 2017

ORODHA YA WADAIWA SUGU WA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU HII HAPA.

Kupata majina ya wadaiwa sugu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  bofya "link" ya hapo chini
Bofya hapa (Click here)

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiwasilisha hoja katika mkutano wa Tano wa Bunge linaloendelea Mjini Dodoma.
Na mwandishi wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na  kutimiza adhma ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Mhe. Maulid Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge unaoendelea Mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...