Rais wa TFF Leodgar Chilla Tenga alitangaza majina ya wajumbe
wanaounda kamati za TFF jana. Walioteuliwa ni pamoja na Jaji Steven Ihema na wakili mwandamizi, Bi. Jesse Mguto walioteuliwa kuziongoza
kamati muhimu za maadili za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
zilizoundwa baada ya kufanyika mabadiliko kwenye katiba ya Shirikisho
hilo mwishoni mwa wiki iliyopita,
Shirikisho hilo pia limemteua Jaji Bernard Luanda kuongoza Kamati ya
Rufaa za Uchaguzi wakati Profesa Mgongo Fimbo ataendelea kuongoza Kamati
ya Rufaa na Kamanda Mstaafu, Alfred Tibaigana akiendelea kuwa
mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu.
No comments:
Post a Comment