Msafara wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda umepata ajali Mkoani Ruvuma mchana wa leo.Katika ajali hiyo mwandishi wa habari mmoja, Afisa kilimo wa mkoa wa Ruvuma wajeruhiwa na magari manne (4) yaharibika .
Msafara ulikuwa ukienda Namtumbo toka Tunduru. Ajali ilitokana na vumbi kuzuia madereva wasione mbele, ilihusisha gari za polisi, Wizara ya Afya.
Na kutoka huko Darfur, hali ya mmoja kati ya majeruhi 14 wa shambulizi dhidi ya vikosi vya JWTZ Darfur yazidi kuwa mbaya, apelekwa Khartoum kwa tiba zaidi, lakini wengine wanaripotiwa kuwa nafuu.
No comments:
Post a Comment