Miamba ya soka ya Ujerumani, Bayern
Munich na Borussia Dortmund leo usiku minamo saa 3.45
inapambana katika fainali ya kugombea
kombe la klabu bingwa barani Ulaya
itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley
mjini London.
Bayern Munich iliitoa Barcelona ya Uhispania
katika nusu fainali na Borussia iliishinda Real
Madrid pia ya Uhispania.Kocha wa Bayern
Jupp Heynckes amesema fainali ya leo ni
fursa yake ya mwisho ya kulitwaa taji la klabu
bingwa za Ulaya-champions League.
Kwa upande wake kocha wa Borussia Jürgen
Klopp amesema ni Bayern iliyojawa shinikizo.
No comments:
Post a Comment